Aliyekuwa mshambuliaji wa Barcelona Neymar amevunja rekodi ya usajili ya wa dunia baada ya kuijunga na PSG kwa ada ya uhamisho wa £200 milioni.
Neymar alikamilisha jana zoezi la vipimo lilifanyika nchini Ureno na tayari amesaini mkataba wa miaka 5.
Mchezaji huyo atapokea kiasi cha £500,000 sawa na shilingi bilioni 1.7 ya kitanzania kama mshahara wake wa wiki.
Timu ya Barcelona ilithibitisha kupokea malipo ya Neymar ambaye ni raia Brazil hapo jana muda mfupi baada ya kufikiwa makubalino.
Neymar mwenye miaka 25 anakuwa mchezaji pekee anayeshikilia rekodi kubwa ya usajili duniani akiwaacha mbali nyota maarufu duniani kama Christiano Ronaldo na Gareth Bale.

Comments
Post a Comment