Neymar anaondoka Barcelona.


Barcelona imethibitisha kuwa mchezaji nyota wa timu hiyo Neymar anataka kujiunga na PSG ya Ufaransa.

Habari kamili imetolewa leo jumatano na timu ambayo imetoa ruhusa kwa Neymar ambaye alishindwa kuhudhuria kwenye mazoezi.

Neymar mwenye miaka 25 alifika asubuhi kwenye mazoezi ya timu hiyo na kuaga baada ya wachezaji ambao alikuwa nao karibu.

Barcelona inajiandaa kumuuza Neymar kwa rekodi ya usajili wa dunia na tayari Meneja wake yupo jijini Paris kwa mazungumzo.

Comments