Kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji John Bocco watakuwa fiti katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC kwa mujibu wa Haji Manara ambaye ni afisa habari wa klabu ya Simba.
Bocco alikosa mchezo wa kwanza kutokana na majeraha na Haruna Niyonzima aliumia uwanjani na kufanyiwa mabadiliko katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting.
Tayari wachezaji hao wameungana wenzao kikosi katika mazoezi ya kujindaa na mtanange huo mkali.
Katika mechi ya kwanza Simba ilishinda mabao 7-0 kwa dhidi ya Ruvu Shooting na mshambuliaji Emanuel Okwi alifunga bao nne peke yake.

Comments
Post a Comment