Njombe Mji yatuma salamu ligi kuu.


Timu ya Njombe Mji ambayo itashiriki ligi kuu msimu huu wamesema kuwa kwa upande wao wamejipanga kufanya vizuri ligi kwa kuwa wana umoja na ushirikiano.

Afisa habari wa timu hiyo, Sofanus Mhagama alisema kuwa kipindi cha mazoezi wachezaji wameonekana kuelewana sana na kuzingatia maelekezo ya mwalimu.

Pia Sofanus aliongeza kuwa Juhudi na umoja ndani ya kikosi cha timu hiyo umeongeza morali kubwa kwa wachezaji ambao wameweka nia ya kuja kufanya vizuri kwenye ligi ya Vodacom.

"Wachezaji wamepewa majukumu na wanasimamiwa vema kuhakikisha wanayatimiza hatuna wasiwasi na yeyote ligi kuu.

"Mwalimu anafarijika sana kwa sababu wachezaji wanajituma na wanazingatia kile anachowafundisha jambo linalotia faraja kwenye timu yetu." Alisema Sofanus.

Comments