Mshambuliaji wa klabu ya Simba Emanuel Anold Okwi amesema kuwa bado ana deni kubwa la kuwalipa mashabiki wa Simba.
Akizungumza jana baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda katika siku ya Simba day Okwi alisema kuwa mashabiki wa simba wanategemea mambo makubwa kutoka kwake hivyo ana wajibu wa kufanya kile mshabiki wanataka.
"Tunawshukuru mashabikiwa Simba, wamejitokeza kwa wingi sana, nami naawambia nina deni kubwa la kulipa, nawaahidi kufanya mambo makubwa msimu huu." Alisema Okwi.
Okwi amewahi kuitumikia Simba kwa mafanikio makubwa na kwa wakati wote amekuwa mchezaji kipenzi kwa mashabiki wa timu hiyo.

Comments
Post a Comment