Beki wa Barcelona Gerard Pique kwa mara ya kwanza amekiri kuwa timu yao imekuwa dhaifu kwa Real Madrid.
Barcelona imekubali kipigo cha mabao 2-0, licha ya Zidane kuwaweka benchi Gareth Bale na Isco na Ronaldo ambaye yupo kifungoni katika mchezo wa jana lakini Barcelona ilishindwa kufurukuta mbele ya Real Madrid.
Barcelona imeambulia goli moja pekee katika mchezo miwili waliyokutana ambalo lilifungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati pale Camp Nou.
"Tuna safari ndefu ingawa bado tunaweza kubadilika, katika kipindi cha miaka 9 nikichokuwa hapa naweza kusema kwa mara ya kwanza tumekuwa dhaifu kwa Real Madrid." Anasema Pique
"Hatupo kwenye kipindi kizuri kama timu kama klabu, tunakiwa kuwa na umoja ili tusonge mbele haraka iwezekanavyo.
"Unaposhindwa unahis mpinzani wako anaweza, ukikumbuka ulivyokuwa bora bila shaka hayo ni masuala ya kiufundi.
"Tulitamani kupata ushindi, lakini hatukuweza." Alimalizia mchezaji huyo
Pamoja na kipindi kigumu wanachopitia lakini Pique ana imani kuna wakati watapata furaha kwenye timu yao.

Comments
Post a Comment