Monaco, PSG zamalizana usajili wa Mbappe.


Paris Saint Germain imefikia makubaliano na Monaco kumsajili mshambuliaji Kylian Lottin Mbappe.

Mbappe atajiunga na PSG kwa mkopo wa mwaka mzima kwa makubaliano ya kumnunua mchezaji huyo kwa dau la usajili wa £166 milioni.

Tayari PSG ilimsajili Neymar kwa kiasi cha £200 milioni akitokea Barcelona hivyo kulingana na usawa wa matumizi kwa mujibu wa UEFA watalazimika kulipa ada ya uhamisho wa Mbappe hapo mwakani.

Mbappe mwenye miaka 18 aliifungia Monaco jumla ya mabao 26 na pasi 6 za magoli katika msimu uliopita.

Comments