RASMI: Chamberlain amesaini Liverpool.


Liverpool imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alex-Oxlade Chamberlain kutoka Arsenal kwa ada ya uhamisho wa £35 milioni.

Mchezaji huyo alikamilisha zoezi la vipimo hapo jana baada ya kuchomoa kuongeza mkataba mpya Emirates.

Tangu juzi mchezaji huyo aliweka wazi kuwa hatajiunga na Chelsea ambayo ilifanya makubaliano ya awali na waajili wake wa zamani.

"Nimefurahi sana kujiunga na Arsenal, siwezi kuongelea furaha yangu, pia sitazungumza sana siku ya leo." Alisema Chamberlain.

Chamberlain amedumu Arsenal kwa miaka 6 akitokea timu yenye kukuza vipaji England, Southampton mwaka 2011.

Comments