RASMI: Gibbs amesaini miaka 4 West Brom.


West Brom imekamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa kushoto wa klabu ya Arsenal Kieran Gibbs kwa ada ya uhamisho wa pauni 7 milioni.

Gibbs mwenye miaka 27 amesaini mkataba wa miaka minne na kukabidhiwa jezi namba 3 na wababe hao wa Howthorns.

Gibbs amedumu Arsenal tangu mwaka 2007 ikiwa ni sawa na kipindi cha miaka 10 na kupoteza namba yake baada ya ujio wa Nacho Monreal.

Mchezaji huyo amekamilisha kiasi cha pauni 38 milioni ambazo zimetumiwa na West Brom baada ya kusajili wachezaji wengine akiwemo Jay Rodriquez aliyetoka Southampton. 

Comments