RASMI: Hazard arejea uwanjani.


Habari njema kwa timu ya Chelsea ni kurejea uwanjani kwa mshambuliaji Eden Hazard ambaye ameikosa michezo miwili ya ligi kuu kutokana na majeraha.

Hazard amekosekana uwanjani kwa muda wa miezi 2 tangu alipoumia enka alipokuwa akiitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amethibitisha kuwa mchezaji huyo ataichezea timu ya vijana chini ya miaka 23 kama sehemu ya kuangalia ufiti wake.

Pia Hazard alishiriki kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Agosti 17 mwaka dhidi ya QPR ambapo Chelsea ilipata ushindi wa mabao 8-0.

Comments