Kiungo Papy Kabamba Tshishimbi ametua nchini na tayari amejiunga na Yanga ambayo imeweka kambi yake visiwani Pemba.
Taarifa za awali zilieza kuwa Yanga ilipoteza mawasiliano na kiungo huyo ambaye hakuwasili nchini kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Lakini baadae taarifa zilieza kuwa tayari mchezaji ametua nchini kusaini mkataba tangu walipokamilisha makubaliano
Taarifa zinaeleza kuwa kiungo ataanza mazoezi mara moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kujindaa na mchezo wa ngao wa jamii ambao unawakutanisha watani hao wa jadi.

Comments
Post a Comment