Ronaldo abeba tuzo ya mwanasoka bora barani Ulaya.


Christiano Ronaldo kwa mara nyingine ameibuka mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanaume barani Ulaya na kutunukiwa tuzo na UEFA.

Ronaldo mwenye miaka 32 aliwapiga bao Buffon wa Juventus na Lionel Messi katika kinyang'anyiro hicho kwa mwaka 2016/17.

                                 Buffon

Ronaldo aliifungia Real Madrid mabao mawili katika fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Juventus na kuwa mchezaji wa kwanza kuandika rekodi ya kuvuka idadi ya mabao 100 barani humo


                          Sergio Ramos

Kwa upande wa mabeki Sergio Ramos ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kuchaguliwa kuwa beki bora wa mwaka na pia kwa upande wa viungo Luka Modrick ndiye aliyeibuka kidedea kwenye tuzo hiyo.

Comments