Sajili 2 kubwa zinazoweza kukamilika leo barani Ulaya.


Tottenham imefikiana makubaliano na PSG kuhusiana na usajili wa beki wa Sergi Aurier kwa ada ya uhamisho wa £23 milioni.

                          Sergi Aurier 

Hadi sasa Sergi Aurier hajapata kibali cha kuishi cha kuishi nchini England jambo pekee ambalo linasumbua mpaka sasa.

Mchezaji huyo alinyanyua maisha yake ya soka katika timu ya Lens, pia alijiunga na Toulouse mwaka 2015 kabla ya kumtika PSG.

Kwa upande wa Arsenal zipo kila dalili huenda beki Shkodran Mustafi akajiunga na Inter Milan kwa mkopo wa mwaka mmoja pia zipo taarifa kuwa huenda Inter Milan ikamnunua mchezaji huyo jumla.

Mustafi alijunga na Arsenal akitokea Valencia kwa ada ya usajili wa pauni 35 milioni.

Wenger anamtazama John Evans ambaye pia anafukuziwa na Manchester City kama mchezaji pekee anaweza kuziba nafasi itakayoachwa wazi na Mustafi.

Comments