Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta nyota yake inazidi kuwaka barani Ulaya baada ya jana kuifungia Genk bao 2 katika ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Antwerp.
Samatta alifunga mabao hayo katika dakika ya 8 na 41 na kuiwezesha Genk kuongoza kwa ushindi wa bao 4-1 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Tayari nahodha huyo wa Taifa Stars ameanza kuwa maarufu kwa mashabiki wa timu na wengine wakidai jezi kutoka na uwezo wake wa kufumania nyavu uwanjani.

Comments
Post a Comment