Mabingwa wa Kombe la FA Simba SC wametoka kifua mbele dhidi ya mpinzani wake Yanga katika mchezo wa Ngao wa Jamii baada ya kushinda kwa penati.
Hadi dakika 90 zinamalizika si Yanga wala Simba ambayo iliweza kutikisa nyavu ya mwenzake.
Mchezaji Juma Mahadh alipaisha penati ya mwisho na kuinyanyua Simba kidedea baada ya Mohamed Ibrahim kufunga mkwaju wa penati wa mwisho.
Licha ya Simba kuonekana kutawala vyema eneo la kiungo lakini Yanga ilijipanga vizuri katika eneo la Ulinzi na kuzuia mashambulizi ya Simba.
Kwa mujibu wa takwimu za Azam Tv Simba ilionekana kutawala mchezo kwa vipindi vyote viwili ambapo katika kipindi cha kwanza iliweza kuongoza kwa umiliki wa Asilimia asilimia 58 na kipindi cha pili kwa asilimia 52.

Comments
Post a Comment