Simba kupitia msemaji wake Haji Manara wametangaza kumpeleka mahakamani beki Pius Buswita ambaye amejiunga na Yanga.
Buswita imefikia uamuzi huo ikiwa ni siku kadhaa baada ya mchezaji huyo kuingia kwenye hatia ya kusaini mkataba kwa timu za Simba na Yanga.
Haji Manara amesema kuwa klabu ya Simva imefikia uamuzi huo baada ya kuona mambo hayendi kiungawana.
"Buswita mwenyewe amekiri kufanya jambo, sijui ni shetani alimpitia au ana sababu zake zake zingine." Alisema Manara
Manara aliongeza kuwa kitendo cha kusambazwa kwa propaganda ambazo zinaonekana kuichafua Simba ndiyo sababu pekee inayowafanya timu hiyo kuelekea mahakani kudai haki yao.

Comments
Post a Comment