Simba waipa tano Yanga usajili wa Tshishimbi.


Klabu ya Simba maarufu kama msimbazi wameonyesha kukubali kuwa Yanga imelamba dume baada ya kumsajili Papy Kabamba Tshishimbi.

Tshishimbi alionesha kiwango kikubwa katika mchezo wake wa kwanza wa ngao ya jamii ambao uliwakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga.

Viongozi na baadhi ya wachezaji wa Simba akiwemo Haruna Niyonzima amewapa tano waajiri wake wa zamani kuwa wamepatia walipofanya usajili wa mkongo huyo.

Kwa upande wa kocha wa Simba Joseph Omog alishindwa kuficha hisia zake kutokana na kuwasifu Yanga kusajili mchezaji mwenye uwezo wa hali juu.

Pia kwa upande wa mashabiki wa Simba hawakuwa nyuma kuwapa hongera Yanga huku wengi wakionekana kukunwa na uwezo wa mchezaji huyo.

Comments