Story 3 za usajili zilizo trend jioni hii barani Ulaya

                                           Thomas Lemar                                                               
Klabu ya Liverpool imeandaa ofa nono ya Paundi 55.5 milioni kumsajili winga wa Thomas Lemar kutoka Monaco.

Hadi sasa haijafahamika endapo Monaco watakubali ofa hiyo au watakataa ili kulinda nguvu ya kikosi chao.

Marcus Rashford

Barcelona inataka kumsajili kinda wa Manchester United Marcus Rashford katika dirisha la kubwa la usajili hapo mwakani. Mpango huo ni kumuandaa mrithi wa Suarez ambaye kwa sasa umri wake unafikia miaka 30.

John Evans

West Brom imekataa ofa ya pauni 21 milioni iliyotolewa na Leicester city kumsajili beki John Evans, pia timu ilichomoa ofa ya pauni 18 milioni ambayo iliwekwa na Manchester city mezani kwa ajili ya beki huyo wiki mbili zilizopita.

Comments