Liverpool imeandaa kiasi cha £136 milioni kwa usajili wa Thomas Lemar kutoka Monaco, Virgil Van Djik kutoka Southampton na tayari wapo kwenye makubaliano na Leipzing kumsajili Naby Keita msimu ujao.
Meneja wa West Brom Tony Pulis anajindaa kupeleka ofa ya £13 milioni kumsajili beki wa Arsenal Kieran Gibbs.
Chelsea imeandaa kiasi cha £75 milioni ambacho kitakamilisha usajili wa Alex-Oxlade Chamberlain na Danny Drink Water kutoka Leicester city.
Crystal Palace, Stoke city na West Brom zipo vitani kumwania mshambuliaji ambaye amekosa makali Tottenham Vincent Janssen.
Beki wa West Brom John Evans anajiandaa kutua Manchester city muda mfupi baada ya kuondoka kwa Eliaqium Mangala ambaye atauzwa kwa mkopo.

Comments
Post a Comment