Timu ya Taifa Stars imerejea kambini na tayari wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana wikiendi hii.
Stars ilianza mazoezi hayo rasmi hapo jana katika uwanja wa uhuru baada ya kocha Salamu Mayanga kutangaza kikosi chake ambacho kitashiriki mchezo huo.
Tayari wachezaji wanaokipiga nje ya nchi wamerejea pia nchini akiwemo Mbwana Samatta wa KRC Genk, Elias Maguli wa Dhofar FC kutoka Oman na Farid Musa anayeichezea Tenerife ya Hispania.
Kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA Taifa Stars wamekubaliana na Botswana kuwa mchezo huo utapigwa nchini katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Taifa Stars
Makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji- Raphael Daudi (Yanga), Kevin Sabato (Adam), Mbwana Samatta (Genk) na Elias Maguli (Dhofar)

Comments
Post a Comment