Mchambuzi wa soka England Andy Townsend ameishauri Liverpool kumwachia Philipe Coutinho na kumnunua Diego Costa.
Liverpool imekataa kiasi cha £90.4 ambayo ni ofa ya pili iliyotolewa na Barcelona kumwachia Phelipe Coutinho.
Mmiliki wa klabu ya Liverpool John Henry alitangaza hadharani msimamo wa timu hiyo kuwa mchezaji huyo hatauzwa popote.
Andy alisema kuwa endapo Liverpool itampiga bei kiungo huyo itakuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutanua kikosi hicho kwa kumsajili fowadi wa
Chelsea Diego Costa na beki Virgil Van Djik ambaye ameonesha nia ya kutua Anfield.
Andy alisema kuwa Liverpool itapata nafasi kubwa kufanya vizuri na kuimarisha kikosi chao endapo itamwachia mchezaji huyo mwenye kiu ya kujiunga na Barcelona.

Comments
Post a Comment