Beki wa Arsenal Kieran Gibbs amemtangulia Alexis Sanchez kutimka Arsenal na kutua West Brom kwa dau la £7 milioni.
Tayari Gibbs amefuzu zoezi la vipimo ambapo anatarajiwa kusaini West Brom muda wowote kuanzia sasa.
Mchezaji huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake kama ilivyo Kwa Alexis Sanchez na Oxlade Chamberlain ambao wapo mbioni kuondoka Arsenal.
Gibbs ameshindwa kuwa chaguo namba moja kwa Meneja Arsene Wenger ambaye anavutiwa zaidi na Nacho Monreal.

Comments
Post a Comment