Timu ya Liverpool imeanza mazungumzo na Arsenal kuhusiana na uhamisho wa kiungo mshambuliaji Alex-Oxlade Chamberlain kwa mujibu wa Sky sports.
Tayari Arsenal ilishafanya makubaliano na Chelsea ambayo iliridhia kutoa kiasi cha pauni 35 milioni lakini Chamberlain amegoma kujiunga na mabingwa hao na kuipendekeza Liverpool.
Chamberlain mwenye miaka 24 amebakiza miezi 11 katika mkataba wake wa sasa na ameshinikiza kuondoka Arsenal ili kupata changamoto zaidi kwenye soka.
Wachambuzi wengi wa soka Akiwemo beki wa zamani wa Arsenal Nigel Winterburn wanaami kuwa chemba amefanyia timu yake kazi ya kutosha na huu muda wake wa kupata changamoto mpya.
Kama Liverpool itafanikiwa kumsajili Chamberlain itakuwa imefanikisha mpango wa meneja Jurgen Klopp ambaye alikuwa akimuhitaji nyota huyo tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa mapema June mwaka huu.

Comments
Post a Comment