Kiungo wa Papy Tshishimbi ambaye alimalizana na Yanga ameshindwa kutua uwanja wa ndege kwa muda ulliotarajiwa.
Waandishi wa habari walikuwa njiapanda baada ya kiungo huyo kushindwa kuwasili katika muda uliopangwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga kiungo huyo alitakiwa kuwasili nchini majira ya saa nane mchana.
Hata hivyo katibu mkuu wa klabu hiyo Bonifasi Mkwasa amesema kuwa mawasiliano baina ya kiungo huyo na wao yalikatika hivyo imekuwa ngumu kufahamu alikuwa wapi.
"Sijui amekwama wapi na atatua saa ngapi mawsiliano kati yetu yamekatika endapo atawasili tutawajulisha." Alisema mkwasa.

Comments
Post a Comment