Usain Bolt apewa ofa ya kucheza soka England.


Mwanariadha maarufu duniani Usain Bolt amepewa ofa ya kujiunga na timu Burton Albion inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Bolt mwenye miaka 30 alitangaza kustaafu rasmi fani yake ya ukimbiaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa mashindano ya IAAF world championship yaliyofanyika London.

Meneja wa Burton Albion amesema kuwa anampa muda mwanariadha huyo kufanya maamuzi juu ya hatma yake kuhusiana na mchezo wa soka.

Bolt ambaye ni Bingwa wa mbio za mita 100 amewahi kucheza soka alipokuwa mdogo kabla ya kuingia kwenye riadha.

Comments