Usajili mwingine wa gharama umefanywa na Everton leo.


Meneja wa timu ya Everton Ronald Koeman amethibitisha kukamilika kwa dili la usajili wa Kiungo Gylf Sirgurdsson kutoka Swansea.

Mchezaji huyo amepasi zoezi la vipimo na tayari Everton imemwaga kiasi cha £45 milioni kama ada ya usajili wa kiungo huyo.

Koeman amesema kuwa mchezaji huyo atakuwepo katika mchezo wa jumatatu ambao Everton itacheza na Man city katika uwanja wa Etihad.

"Sirgurdsson ni moja kati ya wachezaji wazuri sana kwenye ligi, kwa muda mrefu tumehangaikia usajili wake hatimaye tumeweza kufanikiwa." Alisema Koeman.

Comments