Kiungo wa PSG Marco Veratti huenda akawa ameitosa Barcelona kiaina baada ya kukubali kusaini dili jipya wa kwa matajiri hao wa Ufaransa.
Barcelona iliweka mezani ofa ya pauni 60 milioni kama sehemu ya uhamisho wa kiungo huyo ambaye amekuwa akilinganishwa Xavi Hernandez ambaye amewahi kuipa Barcelona mafanikio makubwa.
Veratti mwenye miaka 24 alisema kuwa anafurahia sana maisha ya Ufaransa na ana mapenzi na timu hiyo.
"Barcelona? Hapana bado nitabaki kuwa hapa na nitasaini mkataba mpya, sijafanya makubaliano yoyote na Barcelona." Alisema Veratti.

Comments
Post a Comment