Wajanja wa mitandao nusura wazigombanishe Barca na Madrid.


Real Madrid imetumia siku ya leo kuwaomba radhi mashabiki pamoja viongozi wa Barcelona kutokana na wadokozi mitandao kutumia kurasa yao ya twitter ikionesha klabu hiyo imekamilisha usajili wa Lionel Messi.

Siku kadhaa zilizopita Barcelona iliomba radhi kutokana na tukio kama hilo ambalo limewakuta Real Madrid baada ya kurasa yao kuonesha ilikamilisha usajili wa Angel Di Maria kutoka PSG.

Majira ya saa 11.30 za asubuhi ilioneka posti ambao ilionesha video ya Lionel Messi akiifunga Barcelona na Real Madrid ikimkaribisha.

Posti hiyo iliata jumla ya twits 27000 zikiwa zimepita dakika 45 tu muda mfupi baada kabla ya kuondolewa.

Comments