Wayne Rooney ametangaza kustaafu soka la kimataifa.


Mshambualiaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye timu ya taifa ya England Wayne Rooney ametangaza kustaafu soka la kimataifa.

Fowadi huyo wa Everton ameifungia England jumla ya mabao 53 katika jumla ya mechi 119 aliyoichezea timu hiyo.

Rooney amefikia hatua hiyo baada ya kupokea simu ya kocha wa England Gareth Southgate aliyemtaka kurejea timu ya taifa baada ya kuifungia Everton mabao mawili.

"Nilipokea simu ya Southgate akinitaka kuterejea timu ya taifa ni jambo kubwa sana kwangu.

"Hata hivyo baada ya kufikiria sana nilimwambia Southgate kuwa nimeamua kustaafu timu taifa.

"Limekuwa ni jambo gumu sana kwangu ilinibidi kujadiliana na familia yangu na kuamua kufikia maamuzi hayo.

"Kuichezea England ni jambo lililonipa furaha wakati wote, na kila nilipochaguliwa kikosini na kupewa mikoba ya unahodha nilijiona mimi ni wa pekee sana.

"Lakini nalazimika kusema inatosha kwa sasa nimeamua kubwaga manyanga." Alisema Wayne Rooney.

Comments