Wazir: Nitaisaidia Azam kutwaa ubingwa.


Mshambuliaji mpya wa Azam FC Wazir Junior amesema kuwa anajipanga kupeleka matokeo yatakayopeleka ubingwa kwenye timu hiyo.

Wazir alijiunga na Azam FC kwenye dirisha kubwa la usajili akitoke katika klabu ya Toto Africans ya Mwanza.

Fowadi huyo alisema kuwa ushirikiano mkubwa dhidi ya wachezaji wenzie katika kikosi cha Azam utapeleka matumaini ya ubingwa katika timu ya Azam.

"Kuanza kwa msimu mpya, kwangu nimejipanga kuipelekea timu yangu Ubingwa wa ligi kuu, nitashirikiana vizuri na wenzangu na kuongeza hamasa kikosini." Alisema Junior

Azam kuelekea ligi kuu itakayoanza Agosti 26 mwaka huu, itaelekea Mtwara katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Comments