Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji Alexis Sanchez yupo tayari katika mtanange wa ligi kuu dhidi ya Liverpool wikiendi hii.
Hivi karibuni Sanchez aligoma kusaini mkataba mpya katika timu hiyo jambo ambalo meneja anaamini kuwa haliwezi kupunguza uwezo wa mchezaji huyo uwanjani.
"Yupo na furaha na pia ameweka akili yake kwenye mchezo huo, haimaanishi kwamba hataongeza mkataba mpya kwenye timu hii lakini suala la msingi ni timu kuwa mchezoni na si kufikiria mkataba wa mtu mmoja.
"Alexis anajituma sana, anajitoa, anaonekana yupo tayari kama mwalimu nasema kuwa atacheza kwenye mechi hiyo." Alisema Wenger
Tangu mwanzo wa mwezi Mei mwaka huu mwaka huu Alexis alionesha dalili zote za kutaka kuondoka kwenye timu na kujiunga na Pep Gurdiola ambaye ni kocha wake wa zamani.

Comments
Post a Comment