Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga watalazimika kuingia uwanjani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting bila mshambuliaji Obrey Chirwa.
Chirwa anasumbuliwa na maumivu ya mguu na tayari ameanza kufanyiwa matibabu na wataalam wa afya.
Raia huyo wa Zambia anaungana na wachezaji wengine ambao ni majeruhi kwenye kikosi hicho akiwemo Golikipa Beno Kakolanya na winga wa pembeni Geoffrey Mwashiuya.

Comments
Post a Comment