Yanga kutesti silaha zake Singida Utd kesho


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza baada ya usajili watapiga mchezo kirafiki dhidi ya Singida United kesho katika uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ni sehemu kutesti vifaa vipya kwa mabingwa hao ambao wamesajili wachezaji kadhaa akiwemo Ibrahim Ajib aliyetoka Simba.

Lwandamina alisema kuwa kikosi chake kilifanya kazi ya ziada kujenga ubora wa wachezaji hao kuanzia gym mpaka uwanjani walipokuwa wameweka kambi mkoani Morogoro.

"Mechi hiyo itaniwezesha kutambua wapi tupo imara na wapi tupo dhaifu, kuna wachezaji wapya wamesajiliwa pia, itakuwa ni kipimo na sehemu ya kuchagua yupi ataanza kwenye kikosi cha kwanza." Alisema Lwandamina.

Comments