Yanga yajiandaa kuweka kambi visiwani.


Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara Young Africans wataweka kambi kisiwani Pemba kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya mahasimu yao Simba.

Yanga itaondoka kuelekea visiwani huko siku ya jumapili kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na katibu mkuu wa timu hiyo.

"Tutaelekea visiwani Pemba, kwa sababu hali ya hewa ni nzuri." Alisema Katibu huyo.

Hii itakuwa kambi ya pili kuwekwa na timu hiyo baada ya ile ya kwanza waliyoweka mkoani Morogoro.

Comments