Yanga imemtema mkata umeme.


Mabingwa wa ligi Tanzania bara Young Africans wametangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kiungo mkatabaji wa timu Justice Zulu maarufu kama mkata umeme.

Yanga kupitia katibu wake Charles Bonifas Mkwasa amesema makubaliano yamefikiwa baina ya pande zote mbili na hivyo wameachana na Zulu kwa amani baada kumpigia hesabu malipo yake.

"Tumekubaliana na sasa tutavunja mkataba kupitia makubaliano hayo."Alisema Mkwasa

Zulu amedumu kwa kipindi kifupi kwenye klabu hiyo tangu aliposajiliwa baada ya kutua kwa kocha George Lwandamina.

Comments