Yanga yavutwa shati na Lipuli ya Iringa.


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara wamegawana pointi na Lipuli katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu baada ya kutoka  sare bao 1-1 katika uwanja wa Taifa.

Lipuli ilianza kupata bao kupitia Abdallah Seif aliyefunga dakika ya 44 ya mchezo huo lakini moja baadae Yanga ilichomoa bao hilo kupitia Donald kabla katika dakika ya 45.

Kipindi cha pili Yanga ilionekana yenye kasi zaidi lakini uimara wa beki ya Lipuli ambayo ilikuwa chini ya Nahodha Asante Kwasi.

Katika mechi hiyo Lipuli walipata pigo baada ya nahodha wake kupata Asante Kwasi kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 90.

Comments