Zidane amuweka Bale sokoni.


Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane yupo mbioni kumpiga bei mshambuliaji wa timu hiyo Gareth Bale.

Zipo taarifa kuwa asilimia 70 ya mashabiki wa Real Madrid wanaunga mkono mpango wa kuuzwa kwa nyota ambaye amekuwa akishuka kiwango kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Manchester United ndiyo timu ya kwanza ambayo inavutwa kwenye mtego wa Real Madrid kumsajili nyota.

Mourinho anaitaka Manchester United kuandaa ofa ya £100 milioni kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Hata hivyo Real Madrid inataka kutumia mwanya huo kumsajili golikipa David De Gea.

Comments