Zidane: nina furaha kusaini mkataba mpya.


Kocha wa Real Madrid zinedine Zidane amesema kuwa ana furaha kupewa nafasi ya kusaini mkataba mpya kwenye timu hiyo.

Zidane alijiunga na Real Madrid January mwaka jana baada ya kuondolewa kwa Rafael Benitez na kuiweza timu hiyo kutwaa taji la Mabingwa barani Ulaya mara 2, La liga mara moja na klabu bingwa dunia.

"Historia yangu na Real Madrid ni kubwa kuliko mkataba ana kusaini" alisema Zidane.

"Nina furaha kuhusishwa na klabu hii, mkataba haumaanishi kitu, naweza kusaini miaka 10 au 20 lakini kwa muda mfupi naweza nisiwe hapa.

"Nina furaha sana kwa sababu Real Madrid imenimini kwa kiasi kikubwa." Aliongeza Zidane.

Comments