Asemavyo Mwanjali kuhusu Simba ya sasa.


Nahodha wa klabu ya Simba Method Mwanjali amesema kuwa hakuna wa kuzuia kasi ambayo timu hiyo imeanza nayo msimu huu.

Mwanjali ambaye ni raia wa Zimbabwe anaamini makali ya kikosi yatapeleka makombe mataji yote muhimu kwa wekundu hao wa msimbazi.

"Tumeamua, na sasa tumezamilia kupata mataji yote muhimu, tunaamini katika kasi tuliyonayo, hatutayumba wala kutetereka." Alisema mwanjale.

Akizungumzia kuhusu kikosi cha sasa beki huyo alisema kuwa, huu ni wakati wa Zimbabwe kujivunia kutokana ukubwa wa kikosi ambacho kimesheheni wachezaji walio bora.

"Msimu uliopita hatukuwa na kikosi kipana kama hiki, jambo ambalo lilitugharimu, lakini kwa sasa tuna kikosi kipana kilichosheheni wachezaji bora." Aliongeza nahodha huyo.

Comments