Azam kujipima nguvu na Transit Camp leo.


Klabu ya Azam leo itashuka dimbani kujipima nguvu na Transit Camp katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Mchezo huo maalum ni sehemu ya kuipa nafasi benchi la ufundi la timu hiyo kabla kuelekea mchezo wa ushindani wa ligi dhidi ya SC.

Azam na Simba watakutana katika mchezo ujao kwenye ligi kuu ya Vodacom ambapo kwa mara ya kwanza Azam itatumia uwanja wake wa nyumbani dhidi ya mabingwa hao wa kombe la FA.

Hali ya kukosekana kwa mchezo wa ushindani wikiendi hii kumeifanya Azam kusaka mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya uangalizi wa kikosi chake na kuwapa wachezaji hali ya ushindani.

Azam FC ilishinda mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Ndanda FC bao 1-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Comments