Baada ya kupeleka ofa kadhaa hatimaye Barcelona imekubali kuwa imeshindwa kumng'oa Countinho Liverpool.
Barcelona ilipeleka ofa nne tofauti ili kuishawishi Liverpool lakini hadi dirisha la usajili linafungwa vijogoo hao wa Merseyside hawakuonesha dalili ya kumwachia kiungo huyo.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa thamani ya Coutinho ilikuwa ndogo ikilinganishwa na ofa zilizotolewa na Barcelona isipokuwa timu hiyo haikuwa kwenye mipango ya kumpiga bei Mbrazil huyo.
Pia mmiliki wa Liverpool John Henry aliweka wazi msimamo wa klabu kuhusiana na zuio la kuuzwa kwa nyota huyo.
Barcelona imepata pigo kubwa baada ya kumpoteza Neymar ambaye walimpiga bei katika timu ya PSG ambayo ilitoa kitita cha pauni milion 200.
Coutinho ameonekana jana akiitumikia timu ya taifa ya Brazil na kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Ecuador.

Comments
Post a Comment