Chelsea kumburuza Costa mahakani.


Chelsea imetishia kumpeleka mahakani mshambuliaji wake Diego Costa ambaye amegoma kurejea kwenye timu hiyo mpaka sasa.

Diego Costa amegoma kurejea Stamford Bridge kutokana na mahusiano mabovu kati yake na meneja wa sasa Antonio Conte ambaye alimwambia hayupo kwenye mipango yake msimu huu.

Chelsea imetangaza kumpeleka mahakani mchezaji hiyo, pia wametishia kumpiga faini ya kiasi cha £50 milioni endapo hatawasili mazoezini.

Costa ambaye kwa sasa yupo kwao Brazil aliwalaumu mabingwa hao kutoka na kushindwa kuchukua hatua ya kumpiga bei katika klabu yake ya zamani ya Atletico De Madrid.

Mapema mwezi Mei mwaka huu Costa alipokuwa na kikosi cha Spain alipokea ujumbe kwa kocha Antonio Conte ambaye alimtakia maisha mema baada ya kuweka wazi msimamo wake kuwa hamuitaji mchezaji huyo.

Comments