Mahusiano kati ya Diego Costa na Chelsea yameingia tena shakani baada ya wafanyakazi wa timu hiyo kuondoa sehemu ambayo mshambuliaji huyo amekuwa akipaki gari yake na kuipeleka upande wa timu ya vijana.
Ni muda mfupi tangu Costa amerejea London baada ya Chelsea kutishia kumpiga faini ya kiasi cha pauni 50 milioni pamoja na kumpeleka mahakani.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun bosi wa Chelsea Roman Abromovic ndiye aliyetoa amri hiyo baada ya kukosekana kwa umuhimu wa mchezaji huyo katika kikosi cha kwanza.

Comments
Post a Comment