Coutinho arejea mazoezini tangu kufungwa kwa dirisha la usajili.


Hatimaye kiungo mshambuliaji wa Liverpool Phelipe Countinho amerejea timu hiyo na kuungana na wenzie katika viwanja wa mazoezi huko Mel Wood.

Countinho hajaonekana kwenye klabu hiyo tangu kufungwa kwa dirisha la usajili na kuibukia katika timu ya taifa ya Brazil na kufunga katika mechi ya kimataifa dhidi ya Equador.

Raia huyo wa Brazil alituma barua ya maombi akiutaka uongozi wa Liverpool kumruhusu kujiunga na Barcelona ambayo ilifikia ofa ya tatu yenye thamani ya kiasi cha pauni 118 milioni.

Hata hivyo bahati haikuwa nzuri kwa Coutinho baada ya bosi wa Liverpool John Henry kuzuia biashara ya mchezaji huyo kwa sasa ili kuendeleza maendeleo ya kikosi hicho.

Liverpool ipo mazoezini kujiandaa na mechi kali ya ligi kuu England dhidi ya Manchester City ambayo itachezwa katika uwanja wa Etihad jumamosi ya wiki hii.

Comments