Coutinho atajwa kwenye kikosi cha UCL.


Mshambuliaji wa Phelipe Coutinho ametajwa kwenye orodha ya wachezaji wanaounda kikosi cha Liverpool  ambacho kitashiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Coutinho mwenye miaka 25 aliomba kuhamia Barcelona, lakini Liverpool ambayo ilipokea ofa tatu tofauti iligoma kumpiga bei nyota.

Barcelona ilikuja na ofa ya mwisho yenye kiasi cha £118 milioni lakini hata hivyo Liverpool haikuoneshwa kushtushwa ofa hiyo.

Mmiliki wa Liverpool John Henry tangu awali aliweka wazi msimamo wake kuwa nyota huyo hataondoka kwenye klabu hiyo kwa  sasa.

Raia huyo wa Brazil kwa sasa analitumikia taifa lake kwenye michuano ya kimataifa na atarajea England baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Colombia hapo kesho.

Comments