Beki wa kulia wa klabu ya Simba Shamari Kapombe anatarajiwa kuanza mazoezi jumatatu ijayo baada ya daktari kujiridhisha na hali ya mchezaji huyo ilivyoimarika hivi sasa.
Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa mchezaji huyo ataanza mazoezi mepesi kuanzia jumatatu baada ya kumaliza wiki mbili za nyongeza.
"Kapombe ataanza mazoezi ya taratibu kwa kuwa ndiyo anarajea kwenye mazoezi." Alisema Manara
Kapombe amekuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga kwa muda mrefu jambo ambalo Simba wamoenekana kulivalia njuga ili kumaliza kabisa tatizo la mchezaji huyo.

Comments
Post a Comment