Gyan aifungia Simba, ikiilaza Hard Rock bao 5-0.


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Nicholas Gyan leo ameifungia timu hiyo bao la ushindi katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Hardrock.

Gyan aliifungia bao Simba katika dakika ya 51, huku mabao mengine yakifungwa na Mohamed Ibrahim aliyeifungia Simba mabao mawili, Mwinyi kazimoto pamoja na Said Ndemla.

Simba ilitawala Mpira kwa vipindi vyote viwili kutokana na eneo la kati kutawaliwa vyema na  viungo James Kotei pamoja na Saidi Ndemla.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na mtanange wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC Septemba 6 mwaka huu.

Pia Azam kwa upande wao ilifanya maandalizi ya kujiandaa na mchezo baada ya hapo juzi kucheza mchezo dhidi ya Trans Camp na kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 katika uwanja wa Chamanzi.

Comments