Naodha wa klabu ya Azam Himid Mao amewataka mashabiki wa timu hiyo waje kwa wingi katika uwanja wa Chamanzi Complex wapate kushuhudia ushindi wao dhidi ya Simba.
Himid alisema kuwa wana kila sababu ya kupata ushindi kwenye mchezo ambao kwa mara kwanza Simba itakanyaga katika ardhi ya Chamanzi dhidi ya Azam FC.
"Mimi nawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani watupe sapoti yao ili nasi tuweze kushinda kwa nguvu mchezo huo." Alisema
Nahodha huyo ana imani kuwa kikosi chao kimefanya maandalizi ya kutosha na ushindi ni jambo msingi la kwao bila kujali aina ya mpinzani ambaye watakabiliana nae kutokana morali waliyo nayo kwenye uwanja wa nyumbani.
"Tumejiandaa vizuri, na matokeo ya maandalizi mazuri ni ushindi bila kujali ni nani tunakabiliana naye, tumejiandaa kupata ushindi kwa kuwa tuna morali ya hali ya juu tukiwa nyumbani." aliongeza mchezaji.

efspec0viho Annette Daigle https://www.bettybloomdance.co.uk/profile/Technisches-Zeichnen-Hoischen-Pdf-11-NEW/profile
ReplyDeleteramilosa