Kocha wa Mbeya City Kinha Phiri amesema kuwa anachofikiria kwa sasa kubeba ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Phiri amesema kuwa msimu uliopita alikuwa akitengeneza kikosi hicho ambacho kwa sasa anakiona kipo tayari kwa ushindani.
Raia huyo wa Malawi aliongeza kuwa nia ya klabu hiyo kwa sasa ni kuhakikishia wananyakua moja mataji yaliyopo kwenye ligi ya Tanzania likiwemo taji la FA na kombe la ligi kuu Vodacom.
"Kazi kubwa ilikuwa msimu uliopita wakati naandaa timu ya ushindani lakini kwa sasa nina timu nzuri ambayo ipo imara ingawa si kazi rahisi lakini tumepania ubingwa." Alisema Phiri.
Phiri aliendelea kusema kuwa uwepo wa wachezaji wazoefu na ligi ya Tanzania kama Mrisho Khalfan Ngassa na Ramadhani Chombo Redondo kwenye kikosi hicho ni jambo linalotia faraja ya ubingwa.
"Natarajia kuiona timu yangu ikimaliza nafasi mbili za juu mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika. Tunataka ushindi dhidi ya Ndanda FC pia." Alimaliza kocha huyo.

Comments
Post a Comment