kumbe amesaini mkataba mpya, rais Barca awatoa presha mashabiki.


Rais wa Barcelona Maria Bartomeu amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa tayari mkataba mpya wa nyota wa timu hiyo Lionel Messi ulisaniwa na baba yake mzazi.

Messi amezidisha hofu kwa wapenzi wa timu hiyo baada ya kushindwa kusaini mkataba mpya mpaka sasa ambapo kwa mujibu wa taarifa rasmi staa huyo atamaliza mkataba wake hapo mwakani.

katika mahojiano na gazeti la Diario Sport ambalo hutoka kila jumanne Bartomeu ametangaza kuwa mchezaji huyo atakuwepo Barcelona hadi mwaka 2021 baada ya baba yake mzazi na Staa Gorge kusaini mkataba huo kwa niaba ya mwanae.

"Tumemalizana na ameshasaini, kuna mikataba mitatu." Anasema Bartomeu ambaye anadai mkataba wa awali ulisainia kwenye kampuni ya staa ambaye ni kaka, na mikataba mingine miwili ilisainiwa na baba yake. aliongeza Rais ambaye alisema kuwa baba mzazi wa nyota huyo anayo haki ya kufanya hivyo.

Pia rais huyo aligusia mkataba wa Andres Iniesta ambao unamalizika mwakani ambapo alisema kuwa hawajafahamu maamuzi ya kiungo kama atabaki au ataamua kustaafu soka.

Comments